Shalom

Let glory of our Mighty God covers you all days of your life in Jesus mighty name. Amen.

FANYA CHAGUZI SAHIHI KWA MUNGU.

RUTHU 1:14-18

Kuchagua ya kutenga kitu kimoja miongoni mwa vingine kulingana na umuhimu wa kitu hicho kwako .

Uchaguzi unaweza kuwa mzuri au mbaya kutokana na matokeo yatakayoletwa na kile ulichokichagua

Katika kitabu cha Ruthu 1:14-18 tunamwona mtu moja kutoka Bethlehemu ya Yuda aliyeitwa Elimeleki na mke wake aliyeitwa Naomi pamoja na watoto wake waeili Kilioni na Maloni.

Hawa watu wanne walikimbizwa Bethlehemu na njaa kali wakakimbilia katika nchi ya Moabu, wakakaa moabu hadi vijana hawa wawili wakaoa binti za Wamoabu.

Kilioni akamuoa Ruthu na Maloni akamuoa Orpa. Walikaa moabu kwa muda eElimeleki akafa,Naomi akabaki na watoto wake wawili na wakamwana lakini Biblia inasema walikaa Moabu kwa miaka Kumi Kilioni na Maloni nao wakafa, Naomi akabaki na machungu ya kumpoteza mume wake na watoto wake wawili katka nchi ya ugenini, akiwa katika hali hii ya ujane huku ameachwa na wakamwana ambao bado ni wadogo pia, aliwaza mambo mengi jinsi ya kuwasaidia hawa wakwana, mara akaoata habari kuwa Mungu ameibariki Bethlehemu na chakula kipo cha kutosha.

Naomi akachagua kurudi Bethlehemu, Ruthu na Orpas nao wakachagua kuongozana na Naomi kwenda bethlehehu kumbuka hawa na watu wa Moabu lakini wanaamua kacha nchi yao na kwenda na Naomi katika nchi yake. Ghafla naomi akashtuka akawaambia Hapana niacheni niende mwenyewe maana Mungi hajaniurumia, rudini nyumbani kwenu mkaolewe tena maana mimi nimekuwa mzee siwezi tena kuzaa. Biblia inatuambia kuwa Ruthu na Orpa walilia sana wakamwambia Naomi tutaongozana nawe, Lakini Naomi aliendelea kuwashawishi waachane naye aende meenyewe , ule ushaeishi ulimkatisha Orpa tamaa akaamua kuridi Kwa wazazi wake.

Katika safari ya wokovu kuna watu wenye imani kama ya Orpa wanasimama katika imani lakini wakiyumbishwa kidogo wanakata tamaa haraka na kurudi nyuma na wengine huacha kabisa wokovu. Lakini biblia inatuambia kuwa Ruthu alisimama kidete akwambia Naomi “Usinisihi ikuache nisifuatane nawe maana kila utakapoenda nitaenda, kila utakapo kaa nitakaa, utakapokufa nami ntazikwa hapo watu wako watakuwa watu wangu….

Hebu leo chukua hatua ya imani kama iliyochukua Ruthu ya kuambatana na Naomi kila mahali uambatane na Mungu. Changua leo kutembea na Mungu matatizo yako yote yatakoma kwa Jina la Yesu. Fanya chaguzi sasahihi sasa umwone Mungu atakavyokupigania na kukuvusha katika Magumu yote . Hebu chukua hatua leo na Mungu akubariki.

Ev Jacob Opull Zacharia.

GPH-MINISTRY

Welcome for the online prayer though phone call and Whatsapp call, you can the numbers above

@Ev Jacob Opull Zacharia.